Monday, April 21, 2014

MSANII WA ORIJINO KOMEDI MPOKI AALIKWA UJERUMANI KUHUDHURIA SHEREHE ZA MUUNGANO

 

Msanii maarufu nchini Tanzania Kutoka kundi la Orijino Komedi al maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai anatarajiwa kuondoka nchini mapema mwanzo wa wiki hii kwenda nchini Ujerumani kuhudhuria Mkutano mkuu wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U), utakaoambatana na Kongamano la kibiashara pamoja na Sherehe za Muungano wa Tanzania , zitakazoanza siku ya ijumaa tarehe 25.04.14 na kumalizika siku ya Jumamosi Tarehe 26.04.14.

Mpoki amesema kuwa umuhimu mkubwa wa safari yake ni kuwakilisha wasanii wa Tanzania katika Tamasha hili kubwa la aina yake, na kufafanua kuwa wakati umefika kwa wasanii wa Tanzania kushirikiana kikamilifu na Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kuweza kupata fursa mbali mbali zilizopo huko. 

Amesema amevutiwa sana na Umoja Wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa shughuli zake mbali mbali ambazo umekwishazifanya nchini humo na ameamua kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha (U T U) inafanya vizuri zaidi na kwamba yeye binafsi amekuwa ni mfuatiliaji wa karibu sana wa shughuli za umoja huo.

Mwenyekiti wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha safari ya msanii huyo Maarufu nchini Tanzania, na kusema U T U Ilipendelea sana wasanii zaidi kuhudhuria sherehe hizi lakini kwa bahati mbaya haikuwezekana kutokana na mambo yalio nje ya uwezo wao ingawa UTU ni chombo kinachokubali sana na kuzifagilia kazi za wasanii wa Tanzania.

U T U inamtakia Bw Mpoki Safari njema.

No comments:

Post a Comment