Wednesday, April 9, 2014

ANT EZEKIEL AKWEA PIPA NA KUTUA DUBAI KWA MUMEWEStori: Gladness Mallya
STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amekwea pipa kumfuata mumewe, Sunday Demonte nchini Dubai huku ikielezwa kuwa amefanya hivyo kwa kuhofia kusalitiwa na mumewe.

Aunt Ezekiel katika pozi.
Akiteta na Risasi Mchanganyiko, shosti wa karibu na Aunt alisema: “Yaani amekuwa mpweke sana, anasema hawezi kukaa mbali na mumewe kwa muda mrefu kiasi hicho, anahisi anaweza kuibiwa ndiyo maana amepanga safari ya ghafla, kesho (Alhamisi iliyopita) anaondoka na ndege ya jioni.”
Aunt Ezekiel akiwa na mumewe Demonte.
Paparazi wetu alipomtwangia Aunt na kumpa mchongo mzima, alisema: “Ni kweli kesho (Alhamisi iliyopita) jioni namfuata mume wangu, ukizubaa unaweza kuibiwa hivihivi. Ngoja nikajifariji kwa baby wangu.”
Tangu Aunt aolewe na mumewe Demonte, amekuwa akitumia muda mrefu zaidi hapa Bongo lakini mara kadhaa husafiri kumfuata Dubai.

No comments:

Post a Comment