Monday, March 3, 2014

MLELA AFUNGUKA NA KUDAI KUWA ULEZI NDIO UMENIFICHANa Gladness Mallya
BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, staa wa filamu Bongo, Yusuf Mlela amefunguka kuwa ukimya huo umesababishwa na malezi ya mwanaye.


Yusuf Mlela.
Akichonga na gazeti hili, Mlela alisema anahitaji muda mwingi kukaa na mwanaye Mwantumu kama baba hivyo majukumu yamekuwa mengi, anawaomba mashabiki wake kuelewa kwani ‘soon’ atakuja kivingine.
“Muda mwingi nautumia kukaa na mwanangu hata yale mambo ya kuzunguka hovyo kwenye starehe hakuna tena ila pamoja na malezi bado najiiba kuandaa kazi zangu za filamu na muda siyo mrefu nitaanza kuzitoa,” alisema Mlela.

No comments:

Post a Comment