Monday, March 3, 2014

DIAMOND ANAVYOWACHANGANYA WAREMBO, ONA IDADI KAMILI YA WAREMBO WALIOTOKA NA DIAMOND HAPA

  WALIOSEMA ujana ni maji ya moto hawakukosea. Mkali wao kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni msanii ambaye ana idadi kubwa ya msururu wa wanawake  ambao ametoka nao kimapenzi ambapo, wapo wanaojulikana na wengine hawajulikani.

Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Leo katika makala haya tunakuletea wanawake ambao kwa nyakati tofauti walibanjuka kimapenzi na Diamond ambao kimsingi kutokana na idadi yake, anadhihirisha jina lake la Sukari ya Warembo
Takwimu zinaonesha kuwa karibu kila mwaka jamaa anabadilisha wapenzi ambapo wanawake wamekuwa wakipokezana vijiti.

UPENDO MUSHI ‘PENDO’
Huyu ni msanii wa filamu ambaye alitokea katika Shindano la Maisha Plus. Aliwahi kukiri kwamba alishatoka kimapenzi na Diamond kabla hajawa maarufu kama alivyo sasa, hawakudumu muda mrefu.

WEMA SEPETU
Ni mlimbwende wa Tanzania na msanii wa filamu kwa sasa. Diamond baada ya kupata umaarufu kidogo, alikutana na Wema na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi jambo lililofanya umaarufu wake kuzidi mara dufu.
Wema na Diamond waliachana na kila mmoja akawa anaendelea na maisha yake lakini mwaka jana wawili hao walirudiana na mpaka sasa wapo pamoja.

PENNIEL MUNGILWA ‘PENNY’
Kwa muda huo ambao Diamond aliachana na Wema, ulikuwa ni mwanya wa Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penniel Mungilwa kumiliki penzi la Mbongo Fleva huyo.
Alikuwa ni rafiki wa karibu na Wema, akampindua kwa Diamond. Mapenzi yao yalidumu kwa muda mfupi kabla ya mkali huyo kurudisha majeshi kwa Wema kwa mara nyingine.

ANGEL MAGGY
Diamond wakati akiwa na Wema kabla hawajaachana iliripotiwa kwamba alikuwa akisaliti penzi lao ambapo alitoka kimapenzi na msichana Angel ambaye ni Mkenya lakini hawakukaa muda mrefu, wakamwagana.

JOKATE MWEGELO
Ni mwanamitindo maarufu Tanzania. Penzi lao lilikuwa la muda mfupi na la siri kwani hawakujiachia kama ilivyokuwa kwa Penny na Wema. Huyu naye alikuwa ni rafiki wa Wema lakini alitoka naye kimapenzi ambapo baada ya kuachana, Diamond alimuomba msamaha na kusema alimkosea sana kwani ni mwanamke ambaye alimpenda lakini alimpotezea baada ya kumpata Wema.

JACQUELINE WOLPER
Ni msanii wa filamu Bongo. Wolper na Diamond walitoka kimapenzi lakini waliachana katika mazingira ya kutatanisha jambo lililomfanya Diamond amtungie wimbo kutokana na jinsi alivyoumia.

NAIMA
Huyu alikuwa ni rafiki wa karibu sana wa Wema lakini alitoka kimapenzi na Diamond hali iliyosababisha wanawake hawa kuwa na bifu kwa sababu ya kushea mwanaume huyo mmoja.

REHEMA FABIAN
Huyu ni mrembo aliyeshikilia Taji la Miss Kiswahili ambapo naye aliingia kwenye listi ya kutoka kimapenzi na Diamond. Uhusiano wa wawili hawa haukuwa wa muda mrefu ilikuwa ni kama kupita tu.

NATASHA
Ni mwanadada aliyeshiriki kwenye moja ya video za Diamond. Baada ya hapo habari zilienea kwamba Diamond amempitia ambapo nao hawakukaa muda mrefu.

Baada ya sarakasi zote za wapenzi, sasa Diamond ametulia kwa Beautiful Onyinye, Wema Sepetu! Tutegemee nini? Yetu macho.

No comments:

Post a Comment