Sunday, January 5, 2014

PENNY ''HE, HE, HE YAA.... NAMSHUKURU MUNGU SIKUZAA NA DIAMOND MAANA ANGEWAHARIBU WANANGU SURA PAMOJA NA DOMO KUBWA ''

<>>

Penny  ambaye  ni mpenzi  wa  zamani  wa  Naseeb Abdul "Diamond"   haonekani  kujutia  kitendo  cha  kumwagana    na  msanii  huyo  na  badala  yake  sasa  ameanza  kuzipa  uzito  hoja  za  kumpiga  chini  Diamond  ambaye  walidumu  naye  kimapenzi  kwa  takribani  mwaka  mmoja....
Kwa mujibu wa watu wa karibu  na  Penny, kitendo  cha  Diamond  kumpandisha  jukwaani  Wema  Sepetu  pale Leaders  Club  kilipata  kila  aina  ya  laana  toka  kwa  mama  mzazi  wa  Diamond  kwani  hakuridhia  jambo  hilo.....
"Mama  alilalamika  sana  kuhusu  Diamond  kumpandisha  Wema  pale  leaders  Club, kimsingi  ni  kwamba  hataki  kabisa  uhusiano  kati  ya  Diamond  na  Wema  Sepetu"...Kilisema  chanzo  kimoja ambacho  ni  rafiki  damu  na  familia  hiyo.

Wakati hayo  yakijitokeza  ndani ya familia ya Diamond, kwa upande wa Wema, mama  yake  pia  anadaiwa  kulalamikia  kitendo  cha  mwanaye  kutumika  kila  mara  kumbusti  Diamond  pale  umaarufu  wake  unaposhuka...!
"Mama  Wema  naye  analalamika  mwanaye  kutumika  kama  daraja  la  kuwavusha  watu  kwenye  umaarufu  halafu  wakishafanikiwa  wanamgeuka  na  kumdhalilisha, kifupi  ni  kwamba  hataki  kabisa  kusikia  mahusiano  ya  Wema  na  Diamond"  Kilifunguka  chanzo  hicho.
Aidha  imeelezwa  kuwa  Diamond  amekuwa  akimpgia  simu  Penny  mara  kwa  mara  kumuomba  wayamalize  lakini  Penny amekuwa  akimjibu  kwa  kifupi  kuwa  "Nimekuachia  Wema  Wako"

 Taarifa  nyingine  toka  vyanzo  vya  kuaminika  zinaeleza  kuwa  Penny  amekuwa  akijisifu  kuachana  na  Diamond  kwa  hoja  kuu  tatu:
Moja: Kuondokana  na  skendo  zisizo  na  faida  kwake.
Pili: Kupunguza  malalamiko  toka  kwa  familia  yake.


Tatu: Penny  aliingia  katika  mahusiano  na  Diamond  si  kwa  ajili  ya  mapenzi, bali  kulipa  kisasi kwa  Wema  ambaye  aliwahi  kumchukulia  mpenzi  wake.


"Hata  kutoa  mimba  ya  Diamond  amekuwa  akisema  kwamba  kama  angezaa  naye  watoto  wake  wangekuwa  na  sura  mbaya  na  midomo  ya  ajabu".Kilimalizia  chanzo  hicho

No comments:

Post a Comment