Tuesday, November 26, 2013

TAZAMA PICHA::HUYU NDIYE ALIYE KUWA MBUNGE WA SONGEA ..ANAISHI MAISHA MAGUMU YA KIMASKINI...ANAISHI KWENYE NYUMBA YA URITHI


 Aliyekuwa mbunge wa Songea mjini, Abdulrabi Ali Yusuph(66) akizungumzia maisha yake baada ya kufungwa jela akiwa nyumbani kwake hivi karibuni. Picha na Lauden Mwambona. .  

Aliyekuwa Mbunge wa Songea mjini kuanzia Oktoba 1985 hadi Aprili 1988 alipofungwa jela miaka 11, Abdulrabi Ali Yusuph (66), amesema tangu atoke gerezani hadi sasa anaomba aonane na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ama Rais Benjamin Mkapa na hata Rais Jakaya Kikwete lakini hajafanikiwa hadi leo.
Amesema aliomba nafasi ya kumwona Rais Mwinyi akiwa madarakani ili amweleze ya moyoni, lakini hakufanikiwa na aliendelea kuomba amwone Rais Mkapa hakufanikiwa na sasa anaomba amwone Rais Kikwete bado hajajaaliwa.
Alisema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea ambako anaishi akiwa kwenye nyumba chakavu ya urithi na wake zake wawili pamoja na watoto kadhaa.
Mahojiano ya mwandishi na mbunge huyo yalianza hivi.
Mwandishi: Mheshimiwa habari za siku nyingi. Nimefika hapa kwa niaba ya jarida la Ndani ya Habari linalochapishwa na gazeti la Mwananchi, lengo hasa ni kukujulia hali. Watu wangependa kujua unaendeleaje hasa baada ya kifungo chako. Ningependa kupata maelezo yako juu ya masuala ya maisha ya gerezani na ya sasa ukiwa huru.
Mbunge. Kwanza kabla ya yote. Wewe upo hapa ili uuze gazeti na upate fedha. Je, mimi unanieleza vipi kuhusu mapato hayo.
 Mwandishi: Kazi ya mwandishi siyo biashara, bali ni  ya kijamii. Kazi ya mwandishi ni kuelimisha, kufundisha, kuibua kero na kutaarifu jamii. Kazi ya mwandishi inaweza kukusaidia ama kukuharibia kwa kuibua mambo ambayo unaweza kufanya kwa kuvunja sheria na kuitisha jamii.
Mbunge: Kwa maneno yako haya ni kwamba mimi sina lolote la kufaidika leo?
Mwandishi: Ni kweli sikuja hapa kibiashara bali kukusalimu na kupata hisia zako ama kauli yako baada ya kufungwa jela kwa miaka 11  ukiwa mbunge na sasa upo nje, hivyo tunapenda kujua uliishi vipi jela na jamii inakuonaje baada ya kutoka?
Mbunge:Basi kwa kuwa umefika hapa, nitasema machache, lakini kama utakuja baada ya kujipanga, nitaeleza mengi  mno. Mimi ninazo kero na mambo mengi baada ya kuishi gerezani na kwa kweli nina masikitiko mengi ambayo yananisononesha sana.
Mwandishi:Nashukuru Mheshimiwa, naomba udokeze hisia zako walau kidogo.
Mbunge: Kwanza  ninayo masikitiko mpaka leo kwa viongozi wakuu wa taifa hili. Nasikitika mpaka leo kwa kunyimwa nafasi ya kuonana na walau mmoja kuanzia Rais wa  awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na hata awamu ya nne Jakaya Kikwete
  -MWANANCHI

No comments:

Post a Comment