Thursday, October 17, 2013

PICHA 9 JINSI WATUHUMIWA WA UGAIDI MSITUNI WALIVYOPELEKWA MAHAKAMANI LEO MTWARA


Polisi walijua kabisa msafara wao utakua umewabeba watuhumiwa waliokamatwa kwenye mafunzo ya kijeshi ambayo yalikua yanatolewa kupitia CD za Al Qaeda na Al Shabaab hivyo wakajiandaa kwa ukubwa huu

Taarifa ambazo zimeifikia millardayo.com ni kwamba wale watuhumiwa wa ugaidi waliokamatwa wakifanya mazoezi msituni 88.4 Mtwara, walipelekwa Mahakamani asubuhi ya leo October 17 2013 lakini kutokana na baadhi ya taratibu za kimahakama ikashindikana kupandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mtwara hivyo wakarudishwa mahabusu mpaka hapo itakapoamuliwa ni siku gani wapelekwe tena Mahakamani.

Mwanzoni walikua wamekamatwa 11 tu lakini taarifa nyingine zilizoifikia millardayo.com zinaamplfy kwamba idadi imeongezeka baada ya wengine wawili kukamatwa kulekule walikokamatiwa wengine ambapo hawa wawili hawakukutwa na silaha wala kingine chochote kama ilivyotokea kwa wale wa mwanzo ambao walikutwa na mapanga, silaha mbalimbali pamoja na CD za DVD ambazo zinamafunzo ya kijeshi ya Al Shabaab na Al Qaeda.

Wawili hawa wamekiri kwamba mwalimu wao kule msituni alikua akiwapa mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo kupiga karate, utumiaji wa silaha ambapo pia walikua wakiishi hukohuko msituni kwenye Mapango.Endelea kukaa karibu na millardayo.com na pia unaweza kujiunga kuwa mwanafamilia kupitia facebook.com/millardayo twitter.com/millardayo na instagram.com/millardayo ili kuwa wa kwanza kupata Breaking news, matukio ya michezo, muziki, movie na mengine mbalimbali.Hili hapa juu ndio gari lililobeba baadhi ya hao Watuhumiwa wa ugaidi.No comments:

Post a Comment