Sunday, October 20, 2013

NYAISANGA AKA UNCLE J AFARIKI DUNIA

Julius Nyaisanga a.k.a Anko J (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkongwe Mwenzie,Aboubakar Liongo

HABARI zilizotufikia kutoka mkoani Morogoro ni kwamba Mtangazaji Mkongwe nchini, Julius Nyaisangah 'Uncle J' ameaga dunia. Mpaka mauti yanamfika, Marehemu Nyaisangah alikuwa Mhariri Mtendaji wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro. 

Marehemu Julius Nyaisangah (katikati) akiwa katika pozi na Meneja Mkuu wa GPL Abdallah Mrisho (kushoto)
 Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na katika Kituo cha Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi. Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!  Taarifa zaidi zitawajia baadaye.

No comments:

Post a Comment