Wednesday, October 16, 2013

MUME AMKATA MKEWE MGUU HUKO TARIME MKOANI MARA

Na Waitara Meng’anyi, Tarime

 Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku.

Akisimulua mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake  aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.....BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»

“Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia, baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo  kwa kidole” alisema Ghati.


Wakati anamwonesa lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati hakujuwa kuwa nini kinafuata  alifiki kuwa mambo ya wanaume pengine anataka kwenda   sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama  anataka kuangalia mji kama uko sawa alafu arudi kulala.

“ Alipoipata ile panga akaniambia leo atamitumbua utumbo,  akaanza kunipiga kwa  panga ile  akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa  kulia  ukakatika kama unavyoona” alieleza 
kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala 
kitandani  hospitali ya Wilaya Tarime.

Wakati anafanyiwa ukatili huo ali piga kelele lakini  majirani hawakuwahi kufika  kumsaidia kwa  kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika  maeneo hayo.

“Baadaye walikuja na aliposikia majirani wamefika alikimbia  kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia baisikeli yake, majirani walinifunga mguu

uliokuwa ukivuja damu na kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye  kuletwa hapa” alieleza .

Hata hivyo mwanzoni Ghati alieleza kuwa chanzo cha matatizo hayo yote ni ndoa za mitala na unywaji wa pombe wa mume wake.


“ Nimeishi naye kwa miaka mine sasa na tuna watoto wawili na  tulikuwa tunaishi vizuri, tatizo akinywa pombe huonekana kama amewehuka linguine   ni  baada ya kuoa mke wa pili ambapo   alianza kunichukia , kuanza kunipiga na sasa kunikata mguu” alisema Ghati.


 Ghati hataweza  kurudiana na mume wake huyo  kwa kitendo 
 alichomfanyia kwa vile amesema hakioneshi utu na kuiomba mahakama imuhukumu  
mumewe kifungo jera ili  ajifunze   


kutokana ukatili aliomfanyia.


” Naomba serikali na watu binafsi wanisaidie magongo ya  kutembelea kwa kuwa sasa sina uwezo wa kuyanunua pia wanisaidie kusomesha  watoto wangu maana ni wadogo na mimi ndiye niliye kuwa nikitafuta tunakula”  alisema.

Wananchi walioshuhudia kitendo hicho walionesha  kusikitishwa  na kukilaa kuwa kinaendelea kuharibu jina la na sifa ya Wilaya ya Tarime .


“ Sikifurahii kitendo hiki kwani kinaonesha wazi ukatili wa  hali ya juu kwa binadamu mwenzako  na hii  inasababisha hata watu ambao hawajawahi kufika huku  kutuona  sisi  ni  wanyama kumbe ni watu wachache wanaotuharibia sifa, mahakama imuhukumu huyu mtu   adhabu kubwa inayomstahili ili liwe fundisho kwa wengine” alisema Mwita Machera aliyekuwa  hostalini hapo.

Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa lilifika lilifika  eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha mguu kama inavyoonekana kwenye  picha hapa na kuamru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.

Hata hivyo siku mojs baadaye Chacha Mwita alikamatwa na  jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu nza wananchi ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka hayo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa  polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya 
kuhojiwa Mwiata alikiri kumsababishia mke wake ukilema wa maisha.


“ Vitendo vya kikatili vilishapitwa na wakati,  kumsababishia mtu ukilema wa maisha sii jambo lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna 

ubinadamu kwa watu  japo si wote” alisema Kamugisha kwa nija ya simu.

No comments:

Post a Comment