Thursday, October 3, 2013

DADA KIDOTI ANAUMWA






MWANAMITINDO mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo amefunguka kuwa hali yake kiafya siyo nzuri, anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu.
Akipiga stori na Amani nyumbani kwao maeneo ya Kinondoni
, jijini Dar, Jokate alisema kuwa anasumbuliwa na pumu ambayo huwa inamtokea mara kwa mara ambapo ikimtokea huwa inaambatana na homa kali ambayo inamfanya ashindwe kufanya kazi yoyote.
“Naumwa jamani, pumu inanisumbua inanitesa sana. Inaponitokea huwa nashindwa kufanya kabisa kazi zangu za kila siku na vitu vyote huwa vinalala hadi nitakapopata nafuu,” alisema Jokate kwa tabu.

No comments:

Post a Comment