-
MUSWADA
wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83
umezua balaa bungeni, baada ya wabunge wa Kambi ya Upinzani, bila kujali
itikadi za vyama kutoka nje ya Bunge.
Wabunge waliotoka nje ya Bunge ni wa vyama vya Chadema, CUF na
NCCR-Mageuzi, ambao walikuwa wakishinikiza Muswada huo usisomwe hadi
maoni ya wadau kutoka Zanzibar yapatikane.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza kwa siku ya jana, Mbunge wa
Konde, Khatibu Said Haji (CUF), aliwaongoza wenzake kutoka Chadema,
NCCR-Mageuzi na CUF kutoka nje, huku Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema
(TLP), yeye akibaki ndani ya Bunge.
Dalili za wabunge hao kutoka nje ya Bunge, kama njia ya kuwasilisha
hisia zao kwa Watanzania zilianza kuonekana, baada ya Msemaji wa Kambi
Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Sheria na Katiba, Tundu Lissu, kusema ili
kutimiza matakwa ya Sheria na kwa kuzingatia mapendekezo ya Rasimu ya
Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge linahitaji
kuangalia upya suala la uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalum.
Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 22(2) cha Sheria, idadi ya wajumbe
wa Zanzibar katika Bunge Maalum watatokana na makundi yaliyoainishwa
katika kifungu cha 22(1)(c).
Alisema hali hiyo, ina maana kwamba uchache wa wajumbe Zanzibar,
hawatapungua 55 ambapo Rasimu ya Katiba itakayojadiliwa na Bunge Maalum
inahusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano peke yake.
Rasimu hiyo, imependekeza masuala yote yasiyo ya Muungano ya
Washirika wa Muungano, yaani Tanzania Bara na Zanzibar, yashughulikiwe
na Katiba za Washirika hao.
Lissu, alisema kwa sasa wabunge wanaotoka Zanzibar katika Bunge la
Muungano ni 83, wakati Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina wajumbe 76.
“Kwa ujumla, ili kutekeleza matakwa ya kifungu cha 22(1) na (2) cha
Sheria, Zanzibar itakuwa na wajumbe 219 katika Bunge Maalum lenye
wajumbe 604, sawa na takriban asilimia 36 ya wajumbe wote.
“Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, inataka kujua kama ilikuwa busara na sahihi
kwa nusu ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka Zanzibar, kwa
nini isiwe busara na sahihi vile vile kwa nusu ya wajumbe wa Bunge
Maalum litakaloijadili na kuipitisha Katiba Mpya hiyo kutoka Zanzibar?
“Au
ndio kusema hoja za usawa kati ya nchi Washirika wa Muungano huu ni
kelele za majukwaani tu? Kwa sababu hiyo, na kwa kuzingatia mapendekezo
ya ‘hadhi na haki sawa’ baina ya Washirika wa Muungano yaliyoko katika
Rasimu ya Katiba,” alisema Lissu.
Alisema hali hiyo inawezekana
kwa kuongeza idadi ya wajumbe waliotajwa katika kifungu cha 22(1)(c)
hadi 354, kama ilivyopendekezwa katika maoni ya Kambi ya Upinzani.
Alisema
kwa kurekebisha kifungu cha 22(2) ambacho kitasomeka kwamba, idadi ya
wajumbe kutoka Zanzibar haitapungua asilimia 55 ya wajumbe hao kama
pendekezo hilo litakubaliwa na Bunge.
Alisema wajumbe wa Bunge Maalum kutoka Zanzibar, wataongezeka kutoka 214 kwa mujibu wa Sheria ilivyo sasa, hadi 323.
Rais apingwa
Katika
maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani, imepinga vikali mapendekezo ya
kumwezesha Rais kuteua Wajumbe wa Bunge Maalum wasiotokana na Bunge lako
tukufu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
“Wajumbe
wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba kwa mujibu wa ibara ya
20(2)(e) na (4) ya Muswada Mpya sio, na hawawezi kuwa, wawakilishi wa
wananchi.
“Kwanza, hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala taasisi
zao kuwawakilisha katika Bunge la Katiba kwa sababu Muswada Mpya
unapendekeza wateuliwe na Rais.
“Kwa sababu ya upinzani huo,
mapendekezo ya kumfanya Rais kuwa mteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum
wasiokuwa wabunge na Wawakilishi yaliondolewa katika Muswada huo wa
Sheria hii.
“Badala yake, kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria
iliyotungwa na Bunge lako tukufu kiliweka wazi kwamba “wajumbe mia moja
sitini na sita watateuliwa kutoka kwenye taasisi zilizotajwa,” alisema
Lissu.
Hata hivyo Kambi hiyo ya Upinzani iliingiwa na hofu na
Serikali ya CCM kudhibiti muswada huo kutokana na wingi wabunge kutoka
chama tawala.
No comments:
Post a Comment