Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia kijana mwenye umri
wa miaka 15 mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari
Kelamfua ya wilayani Rombo baada ya kukutwa akimwingilia ndama wa
ng’ombe.
Akithibitisha, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema tukio hilo lilitokea Agosti 3 mwaka huu saa 5:10 usiku nyumbani kwao Kelamfua ambapo baba wa kijana huyo ndiyo aliyemfumania kwa kuwa alikuwa akimfuatilia kwa muda mrefu na ndipo alipomkamata.
Alisema kuwa kabla ya tukio hilo kijana huyo aliwahi kukutwa akifanya mapenzi na kuku na kuanzia hapo

mzazi wake huyo akaanza kumfuatilia.
Kamanda alisema kuwa baada ya kukamatwa kijana huyo alifikishwa kituo cha polisi na kuhojiwa ambapo alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa amekuwa akitafuta wasichana bila mafanikio. Aidha aliongeza kuwa kila msichana anayemtakia neno la mapenzi amekuwa akitaka fedha nyingi wakati yeye ni mwanafunzi hana uwezo wa kupata fedha.
Boaz alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa ajili ya taratibu nyingine. (HabariLeo)

No comments:
Post a Comment