Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Mikoa na Vikosi.
Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mtwara Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa ambaye
amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi na nafasi yake
inachukuliwa na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe
Stephen kutoka Makao Makuu ya Polisi.
Aidha, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Viwanda vya ndege Kamishina
Msaidizi (ACP) Deusdedit Kato amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na
nafasi hiyo inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Selemani
Hamisi kutoka Makao Makuu Idara ya Upelelezi.
Wengine ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad anayeenda
kuwa Mkuu wa Upelelezi Viwanja vya ndege ambapo hapo awali nafasi hiyo
ilikuwa inashikiliwa na David Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD).
Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment