Madam Rita
Mratibu
wa shindano la Epic Bongo Star Search(EBSS) Rita Paulsen (Madam Rita)Amesema hatamfungulia mashitaka Ney wa Mitego kwa kuwa hatakuwa na pesa za kumlipa kwa maana itakuwa kesi ya
kumchafua na inaweza kumgharimu pesa nyingi.
.
Madam Rita ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano
katika kipindi cha burudani cha The Strengo Saturday kinachorushwa na
Radio Victoria fm kupitia 90.6 kilichopo Musoma, Mara. Ambapo mtangazaji
wa kipindi hicho Patrick Derrick Mwankale alitaka kujua sababu kubwa ya
EBSS kuhamishiwa katika kituo cha televisheni cha TBC1 ikitokea ITV na
vipi kuhusiana na habari zilizopo za yeye (Madam Rita) kutaka
kumfungulia Nay Wa Mitego kesi ya kumchafua . " unajua patrick
nashangazwa sana na hizi taarifa zilizopo katika mitandao ya kijamii
pamoja na vyombo
vya habari, mimi sina mpango wa kumfungulia kesi mahakamani maana mimi
ninajua anatafuta kick kupitia jina langu , anatafuta kuendelea kukaa
katika soko la muziki kupitia jina langu, nikimfungulia kesi ya
kunichafua mimi hatakuwa na hela ya kunilipa kabisa na kwanza nitakuwa
napoteza muda wangu wa kusumbuana naye nakuzidi kumuweka juu zaidi.
unajua mimi kwanza hata simfahamu, sijawahi kukutana naye, sijawahi hata
kukaa nae na hapo ndipo nitalazimika kumtafuta ili nimjue, lakini kuhusu
kumfungulia kesi siwazi kabisa maana hana hela ya kunilipa huyo" alisema
Madam Rita
Madam Rita
akionekana kuumizwa zaidi na taarifa hizo, amesema , huyo msanii ni kati
ya wasanii wasiojitambua kabisa wala kujielewi. Maana kabla ya kuimba
chochote anatakiwa kufanya reasech ya kutosha na siyo kuropoka ujinga
kujitafutia kick , kwa kuwa hata watanzania pamoja na wasanii wenyewe
wanamshangaa kwa hayo anayosema na kuimba. Kila mtu anajua kuwa hela na
zawadi zinazotangazwa zinatoka na siyo propaganda
na kama ni swala la msanii kutokusikika au kuvuma baada ya yeye kutolewa
na shindano hilo hiyo ni juu yake binafsi.
Pia alisema hakuna sababu kubwa sana iliyopelekea EBSS ya mwaka huu
kuhamishiwa TBC1 zaidi ya maslahi ya kibiashara .Na pia ndio channel
ambayo hivi sasa ina watazamaji wengi kutokana na ishu ya ving'amuzi
kwasababu ITV kuna baadhi ya mikoa haikamati kwa sababu ya ishu hiyo ya
ving'amuzi.
No comments:
Post a Comment