
John Obi Mikel ameanza kufanya mazungumzo na Galatasaray (HM)

Obi na Drogba wakiwa pamoja Chelsea enzi hizo
KLABU ya Galatasaray ya Uturuki
imefufua mazungumzo na Chelsea na ipo tayari kutoa Pauni Milioni 16
kumnunua kiungo Mnigeria, John Obi Mikel.Mtaalamu huyo aliungana na The Blues mwaka 2006 - akisajiliwa na Jose Mourinho - baada ya mzozo mkubwa wa usajili uliozihusisha Manchester United na Lyn Oslo ya Norway.
Lakini anaweza kuondoka ikiwa ni miaka sita, baada ya kocha huyo kurejea.
Dili hilo litafanya Mikel aungane tena Didier Drogba, ambaye amejiunga na Galatasaray msimu uliopita baada ya kuondoka Chelsea kuhamia Shanghai Shenhua ya China.
Mikel amebakiza miaka minne katika Mkataba wake Stamford Bridge, lakini akiwa kwenye Kombe la Mabara na Nigeria alisema mustakabali wake ni tata.
"Nina miaka minne katika mkataba wangu na Chelsea, lakini unafahamu, katika soka huwezi kubashiri, siku moja upo hapa, siku inayofuata unaweza kuondoka,"alisema. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment