Wednesday, June 19, 2013

WABUNGE WA CHADEMA WANAELEKEA MAHAKAMANI ARUSHA MUDA HUU


Mtakumbuka kuwa jana wabunge wa chadema pamoja na waombolezaji wengine zaidi ya 70 walikamatwa na jeshi la Polisi kwa kile kilichoitwa kukusanyika bila kibali walipo kuwa uwanja wa SOWETO kwa ajili ya kutaka kuaga miili ya wahanga wa mabomu.

Wabunge hao wa CHADEMA ndio wanapelekwa mahakamani muda huu.


Ni Tundu lissu (Singida Mashariki), mustafa Akonay (Mbulu), Mbunge wa Mpanda ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA bara, Mzee Said Amour Arfi pamoja na mbunge wa viti maalum Joyce Mukya wa Arusha.


Yupo pia afisa habari wa Chadema bwana
Tumaini Makene.

• Mashtaka ni mkusanyiko usio kuwa halali


• Zaidi ya waombolezaji 70 pia wamepelekwa mahakamani kwa makosa ya kukusanyika bila kibali.


» Tutaendelea kujuzana yanayojiri.



Quote By sokoinei View Post
Nipo hapa Kituo cha polisi Kati Arusha,nawaona Wabunge wa CDM na baadhi ya Kina mama wamepandishwa kwenye Karandinga saa 6:24.
Wa kwanza kupanda ni Mh Tundu Lisu akafuatiwa na Said Arfi na Mustafa Akunay.

Wamekalishwa chini kwenye Karandinga ni zaidi ya dk 30 sasa gari lipo tu halijaondoka na hawajapandishwa watu wengine isipokua Wabunge hao watatu diwani wa daraja mbili mgombea udiwani wa Kimandolu Mch Ngowi na baadhi ya kina mama kama sita hivi.

No comments:

Post a Comment