Jumamosi ya June 8 ilikuwa ni ya kihistoria kwa muziki wa Tanzania kwakuwa pamoja na kutolewa tuzo za KTMA, wasanii wawili, Noorah na H.Baba walifungua ndoa na kuisaliti rasmi kambi maarufu mjini ya makapela.
Noorah akiwa na mke wake
Harusi ya Noorah ilifanyika mkoani kwao Shinyanga na ameiambia Bongo5 kuwa ilienda vizuri na kila mmoja alifurahi.
“Kwangu mimi kiukweli ni ya kihistoria sana kwasababu kila mtu alikuwa happy. Unajua shughuli kama hii ni ya watu wengu, shughuli ikiwa na watu wengi halafu watu wote wakafurahi inakupa faraja kubwa sana hata wewe mwenyewe,” amesema Noorah ambaye mke wake anaitwa Camilla.
Noorah akiwa amembeba mke wake
“Ndoa ni commitment, ndoa ni majukumu, ndo ni vitu kama hivyo sasa kama nimefika hatua ya kuweza kudiriki kuthubutu kitu kama hicho maana yake najiona kwamba nimekomaa vizuri.”
No comments:
Post a Comment