Monday, June 17, 2013

SHIRIKA LA WORLD VISSION WILAYA YA BABATI KUPITIA MRADI WAKE WA GOROWA ADP LATOA MSAADA WA KUKU 500 KWA WANAKIJIJI

 Na Elisante William
 Shirika la WORLD VISSION Mkoani Manyara wilaya ya Babati imetoa misaada Mbalimbali ikiwemo vifaa vya Hosipitali pamoja na Kuku 500 kwa wanakijiji wanao hudumiwa na Mradi huo,

Akizungumza katika Utoaji wa Misaada hiyo, Mratibu wa Mradi huo Bw, Daudi Charles alisema kuwa lengo la kutoa misaada hiyo ni ili wanakijiji hao wakwamuke kiuchumi jambo ambalo litawasaidia watoto wa wanakijiji hao, wasipate shida na waweze kupata haki zao za kimsingi.


Hapa ni Mratibu wa Mradi wa Gorowa ADP (katikati) bw, Daudi Charles akimkabidhi vifaa vya Hosipitali Muuguzi Neema Niilo, wa Zahanati iliyopo katika kijiji cha Endagwe.Zahanati hiyo ilipatiwa viafaa kama Mavazi ya Wauguzi, Sabuni, Vifaa vya Kuzalishia na vingine vingi.

Hapa Muuguzi, akivalishwa vazi litakalo msaidia wakati anahudumia Wagonjwa.

Miongoni mwa Kuku 500 ambao wanakijiji walifaidishwa na Shirika la WORLD VISSION kupitia mradi wake wa GOROWA ADP ambapo kila mwanakijiji alipatiwa kuku wawiliwawili ambapokabla ya kupatiwa Kuku hao wanakijiji walipatiwa Mafunzo juu ya namna ya kuwafuga kuku hao.

Kila Mwananchi aliepata Mafunzo alipewa kuku wawili.

Wanakijiji wakifurahia Kuku kutoka kwa World Vission

No comments:

Post a Comment