MWANA FA |
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Mwana FA
anafikiria kuahirisha shoo yake ya kesho kufuatia kifo cha msanii mwenzake wa
kizazi kipya Langa Kileo, kilichotokea leo jijini Dar es Salaam.
Mwana FA anafikiria kuahirisha shoo yake ya kesho iliyopangwa kufanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na tayari ameanza kuwasiliana na meneja wake kwa ajili ya hatua hiyo.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Mwana FA kuahirisha shoo yake,
awali ilipaswa kufanyika Mei 31 mwaka huu lakini ikaahirishwa kutokana na kifo
cha aliyekuwa msanii mwenzake wa Bongo Fleva Albert Mangwea.
Hata hivyo Mwana FA ametoa tahadhara ya kejeri juu ya hatua hiyo
huku akimtupia madongo mhasimu wake mkubwa Mwanadada Lady Jay Dee...
Katika
taarifa yake aliyoitupia katika mtandao wa kijamii wa Facebook Mwana FA amesema
kwamba:
7 minutes ago via mobile · Like Mwana FA Halisi : "Msiba wa mwana HIPHOP mwenzetu Langa unanifanya nifikirie kuahirisha show ya kesho. Nawasiliana na manager wangu kisha nitawajuza ,but si kwa kumuogopa mwanamke,Let it be clear"

No comments:
Post a Comment