Saturday, June 22, 2013

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA 
NA USTAWI WA JAMII
 NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, anapenda kuwaarifu Wataalamu wa Kada za Afya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi kutokana na maombi ya kazi waliyowasilisha kwake kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Watalamu wote wanatakiwa kuripoti katika vituo walivyopangiwa kabla ya tarehe 30 Juni, 2013. Baada ya muda huo kumalizika waajiri wanatakiwa kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu  Wizara ya Af
ya na Ustawi wa Jamii ili wale ambao  hawajaripoti nafasi zao ziweze kujazwa.

Aidha, Waajiri wote wanakumbushwa kukagua vyeti halisi (Original) vya kidato cha nne na kidato cha Sita pamoja na vyeti vya taaluma kabla ya kuwaajiri wataalamu hawa wa kada za afya.

Orodha ya majina ya Wataalamu waliopangiwa kazi na vituo walivyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz Wizara haitatoa barua za kupangiwa vituo vya kazi kama ilivyokuwa hapo awali.

Nawapongeza kwa kupata nafasi hii ya kutumia utaalamu wenu katika kuwahudumia wananchi, na ninawatakieni kazi njema na utumishi uliotukuka.

No comments:

Post a Comment