Monday, June 17, 2013

MPAMBANO WA NGUMI KATI YA HALIMA MDEE NA JACKLINE WOLPER WAPAMBA MOTO


Mbunge wa Kawe (Chandema), Halima Mdee ameanza maandalizi yake ya pambano la ngumi dhidi ya staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper.
Pambano la wakali hao litafanyika Julai 7, siku ya Sabasaba katika Tamasha la Matumaini kwenye Uwanja we Taifa jijini Dar es Salaam.
Mdee amekuwa akiendelea na mazoezi yak echini ya Mbunge wa CCM, Idd Azzan ambaye pia siku hiyo atapanda ulingoni kutoana jasho na mkali wa Bongo Movie Jacob Steven ‘JB’

Katika tamasha hilo mwaka jana Wolper alionyesha uwezo kuliko Wema Sepetu katika pambano lao lililosisimua.
Lakini Mdee ametamba kumpoteza Wolper katika pambano lao hilo la Julai 7.
Mdee anaendelea na mazoezi mjini Dodoma, wakati Wolper anaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam.
CHANZO CHA HABARI HII NI SALEHJEMBE.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment