Thursday, June 20, 2013

KIONGOZI WA CHADEMA ALIYEFARIKI KWA BOMU LA ARUSHA AZIKWA HUKO ARUSHA...!!

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakimpumzisha Judith katika nyumba yake ya milele, Judith William Moshi alikuwa ni katibu wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha na aliuawa katika shambulio la bomu lililotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, Soweto Arusha.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi (SUGU) wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Judith William Moshi aliyekuwa katibu wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha,Judith aliuawa katika shambulio la bomu liliotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, Soweto Arusha.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Judith William Moshi aliyekuwa katibu wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha, Judith aliuawa katika shambulio la bomu liliotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, Soweto Arusha.
Baadhi ya Viongozi wa Chadema na wakazi wa Arusha wakiwa katika mazishi ya marehemu Judith William Moshi aliyekuwa kiongozi wa CHADEMA kata ya Sokon 1, Judith aliuawa katika shambulio la bomu lililotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, Soweto Arusha.
Baadhi ya Wabunge ,Viongozi wa Chadema na wakazi wa Arusha wakiwa katika ibada ya mazishi ya marehemu Judith William Moshi aliyekuwa kiongozi wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha, ibada ya mazishi ilifanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Sokoni 1 na kuzikwa katika makaburi ya Sokon 1. Judith aliuawa katika shambulio la bomu lililotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, Soweto Arusha.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (kulia) na Mbunge Grace Kiwelu (viti maalumu Moshi) wakiwa mstari wa mbele na wabunge wengine wakiongoza kubeba jeneza la Marehemu Judith William Moshi aliyekuwa kiongozi wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha, ibada ya mazishi ilifanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Sokoni 1, Judith aliuawa katika shambulio la bomu lililotokea katikamkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, Soweto Arusha.

No comments:

Post a Comment