Wapo wanaomuunga mkono Rais Kagame na wapo pia wanaompinga kwa kauli yake...
Rais Kagame alimtukana Rais Kiwete kwa kuita ushauri wake kwamba ni ushauri wa kijinga kwa wanyarandwa,awali Rais Kikwete alizishauri nchi za Rwanda na Congo DRC kukutana na kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati wa mkutano wa kujadili amani na mpango wa ulinzi nchini Congo DRC uliofanyika katika Makao Makuu ya AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Katika ushauri huo Rais Kikwete alisema kwamba ni vyema Rais Kagame akakaa katika meza ya mazungumzo ya amani na Rais wa Congo DRC Joseph Kabila ili kumaliza tofauti zao badala ya kutumia nguvu ya kijeshi.
“Nimekaa kimya kwa kipindi kirefu na kwa jinsi nilivyoweza kwa sababu nilifikiri kwamba mazungumzo ya kipuuzi yaliyozungumzwa na watu wajinga yamemalizika "alisema Rais Kagame.
Katika hatua nyingine Rais Kagame alisema kwamba ushauri huo wa Rais Kikwete ni sawa na kuwachezea wanyarandwa mbele ya mataifa.
No comments:
Post a Comment