Tuesday, May 7, 2013

WAZIRI MKUU -PINDA KUEPELEKA DAWA ARUSHA KATIKA HOSIPITALI YA MOUNT MERU NA KUWATEMBELEA WAHANGA WA BOMU LILILOLIPUA KANISANI


pinda a505d
Mahmoud Ahmad Arusha
Waziri mkuu Pinda kukabidhi Madawa yenye thamani ya Tsh.16.2 milion kwa Hospitali ya mkoa mount Meru wakati atakapowatembelea wagonjwa walipata majeruhi kwenye muendelezo uliotokea jana wa  mlipuko wa bomu kwenye Kanisa la Mtakatifu JosephMfanyakazi  eneo La olasiti Nje kidogo ya Jiji la Arusha.
 Akizungumza wakati akitoa Mablanketi kwa niaba ya wizara ya utalii kupitia shirika la hifadhi la taifa (TANAPA)Naibu waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alisema kuwa wizara yake kupitia Tanapa wametoa vifaa hivyo ili kusaidia hospitali hiyo yenye huba wa madawa na vifaa mbali mbali ikiwemo upungufu wa vitanda,madawa na mablanketi ambayo sehemu ya madawa itakabidhiwa jioni na Mh.waziri mkuu kwa niaba ya serekali.



 “Kwanza tunatoa pole kwa majeruhi wote waliopatwa na tukio hilo na tunawatakia wapone haraka pili msaada huu tunautoa kwa ajili ya kupunguza upungufu uliotokea kwenye hospitali yetu ntakaa na wenzangu wadau wa utalii tuangalie nini cha kufanya” alisema nyalandu.
 Alisema kuwa jumla ya tsh.16.2 milion zitatumika kununulia madawa ambayo ya takabidhiwa jioni na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Peter Pinda.
 Wakati huo huo kijana wa miaka 16 mkazi wa Olasiti James Gerald amefariki dunia usiku wa kuamkia Leo ikiwa ni mtu wa pili kufariki katika tukio la mlipuko wa bomu uliotokea kwenye kanisa la Joseph Mfanyakazi kwenye kata ya Olasit jijini Arusha,
 Akithibitisha kutokea kwa mauti hayo Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Mount Meru dkt.Mariam Murtazah alisema kuwa hospitali hiyo ilibidi kuongeza dawa kutokana na wingi wa watu na kuwa msaada waliupata umekuja wakati muafaka kwani hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa vifaa yakiwemo madawa.
 Aidha Askofu mkuu wa JImbo kuu la katoliki Arusha Josephat Lebulu Akiongozana na Balozi wa Vatikan hapa nchini Fransisco Padilla waliwatembelea majeruhi wa mlipuko wa mabomu majra ya saa 11;39 na kuwafariji majeruhi hao kwa kuwawekea mkono wa Baraka kwenye mapaji ya uso.
 Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka kuwatembelea majeruhi hao alisema wamepata salamu mbali mbali kutoka mataifa mbali mbali wakiwatakia majeruhi hao wapone haraka na rambi rambi kwa wafiwa huku akitoa tamko la kanisa kuwa ni mafundisho ya bwana yesu kuwa tuushinde ubaya.
 Lebulu aliwataka wakirsto hapa watanzania kuweka ulinzi wao moyoni badala ya kutegemea polisi kwani majaribu ya shetani ni mengi kama unavyoona shetani anatumia watu kupiga mabomu hadi kwenye nyumba za ibada,hata ukiweka ulinzi kwenye nyumba za ibada bado shetani ataendelea kuwatumia wafuasi wake.
 “Tuweke ulinzi rohoni mwetu kwanza kabla ya kuuweka mbele ulinzi wa Askari wetu hakika kama hatutatumika na shetani basi matukio kama haya yatakuwa historia”alisema Lebulu mbele ya balozi Padilla

No comments:

Post a Comment