Akizungumza katika Mkutano uliowajumuisha Wanawake kutoka katika Masoko Mbalimbali jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Equality For Growth Bi Jane Magigita amesema kuwa katika Utafiti uliofanywa na Shirika lao, wamebaini kuwa wanawake wanafanya kazi kwenye Mazingira Magumu ikiwemo Matusi na Uzalilishwaji.
Amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtu kuhakikisha kuwa Mwanamke anaheshimiwa na kupatiwa haki yake ya Msingi na sio kumdharau na kumdhalilisha.
Ameendelea kusema kuwa, viongozi wa Masoko wanapaswa kuchukua hatua kali endapo watabaini Mfanyabihashara au mteja ametoa lugha ya Matusi ya Kumdhalilisha Mwanamke.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wanawake la Equality for Growth Bi Jane Magigita akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari nje kidogo ya Mkutano huo. |
Baadhi ya Wanawake wakipatiwa Semina |
No comments:
Post a Comment