Wednesday, May 1, 2013

MAGOROFA YALIYOJENGWA BILA KIBALI KATIKA MANISPAA YA KINONDONI KUBOMOLEWA, WAJENZI WA MAGOROFA HAYO WAPEWA MIEZI MITATU KUJISALIMISHA:::: MEYA

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe, Yusuph Mwenda , akizungumza mbele ya Waandishi wa   habari  (hawapo pichani) leo wakati alipotembelea jengo lililojengwa pasipo kibali katika maeneo ya Manzese Jijini Dar es Salaam.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw Yusuph Mwenda amewataka wamiliki wa Majengo yanayojengwa bila kibali katika manispaa hiyo kujisalimisha ndani ya miezi mitatu ili kupata kibali cha kuendelea kujenga Majengo yao.

Mwenda amesema kuwa, wananchi nao wanatakiwa kutoa taarifa wanapo ona kuwa kuna ujengwaji wa  holela wa Majengo katika Manispaa hiyo.

"Kama mwananchi ameona kuna jengo lina jengwa na hakuna kibao chochote cha kuonyesha uhalali wa jengo hilo, atoe taarifa katika ofisi ya Serikali ya Mtaa au katika Manispaa ya Kinondoni ili hatua Zichukuliwe Mapema", Amesema Meya.
Hili ni Ghorofa lililokaguliwa leo na Meya wa Manispaa ya Kinondoni linalomilikiwa na Mtu aliyefahamika kwa jina moja  Dkt, Mambo ambapo alitoa amri ya kusitishwa ujenzi wa Jengo hilo.

Mkandarasi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni akifafanua jambo mbele ya Viongozi waliokuwemo wakati wa kusitishwa kwa ujenzi wa Jengo hilo.

Hili ni shimo lililokuwemo katika Jengo hilo


No comments:

Post a Comment