Wednesday, May 29, 2013

LHRC YAITOA RIPOTI KAMILI JUU YA MGOGORO WA GESI ULIOPO MTWARA

Kaimu Mkurugenzi wa  Mtendaji wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu Bw Horoild Sungusha akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao makuu ya Kituo hicho juu ya Wito wao kwa wananchi na Serikali kutokana na Mgogoro wa Gesi uliopo Mkoani Mtwara.
 Kituo hicho kimetoa wito  kwa wananchi wa Mtwara na Mikoa Mingine kuepuka kujichukulia Sheria Mkononi badala yake wazingaie taratibu za kisheria katika kudai haki zao na kituo kitakuwa tayari kutoa msaada wa sheria pale haki za wananchi zinapo vunjwa ili kudumisha utawala wa Sheria.

Hata hivyo kituo hicho kimeishauri serikali na viongozi wake kuhakikisha kuwa  wanawashirikisha Wananchi wa maeneo yote yenye Rasilimali kuanzia kwenye Mipango, utafiti, Utekelezaji na Utathmini wa miradi inayofanywa na Kupangwa kufanywa katika Maeneo hayo ili wananchi wawe na Taarifa sahihi za wakati na kina juu ya Miradi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi akijadiliana jambo na Timu nzima iliyokwenda kufanya Utafiti juu ya Mgogoro wa Gesi uliopo mtwara

Hii ndiyo Timu nzima kutoka Kushoto ni Pasiance Mlowe ambaye ni Mwanasheria, Kaimu Mkurugenzi wa LHRC Harold Sungusia.

No comments:

Post a Comment