MWENYEKITI wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage pamoja na viongozi wengine wa klabu hiyo wanatarajiwa kwenda nchini uingereza kwa ajili kukutna na uongozi wa klabu inayoshiriki ligi kuu ya England, Sunderland AFC .
Safari hiyo ni matunda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliwaunganisha Rage na mwenyekiti wa Sunderland, Ellis Short aliyekuja nchini mapema mwaka huu.
Katika mkubaliano ya awali ya ushirikiano na udhamini, Sunderland imepania kuwekeza katika soka la vijana na itakuwa ikichukua wachezaji katika makundi na umri tofauti wa klabu ya Simba na kwenda kujifunza katika taasisi yao ya vijana.
Na tayari wachezaji chipukizi wa Simba, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Shomari Kapombe wameshateuliwa kwenda kufanya majaribio katika kituo maalum cha vijana cha klabu hiyo ambapo watakwenda huko mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom.
Pamoja na kupatiwa mafunzo maalum katika kituo cha kulea vijana cha timu hiyo, kama watafanya vema katika mazoezi yao huenda wakasajiliwa kuichezea timu ya vijana ya Sunderland
No comments:
Post a Comment