Sunday, April 21, 2013

SERIKALI YA TANZANIA YAPOKEA SH BILIONI 18.42 KWAAJILI YA MIRADI YA MAJI KUTOKA KWA OFID


 Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa akisaini mkataba wa maji ambao utawasaidia wananchi ya Manyara.
 Waziri wa Fedha Dkt Wiliam Mgimwa akipokea mkataba kutoka kwa mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrck Pima.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akibadilishana mkataba na Mkurugenzi  wa OFID kushoto ni Katibu wa Waziri wa Fedha Bw. Omar Khama akiwasikiliza wafanyakazi wa OFID.

Serikali ya Tanzania yasaini mkataba wa jumla ya dola za kimarekani milioni 16 kusaidia mradi wa maji Orkesumet mkoani Manyara. Mkataba huo umesainiwa  leo kati ya Serikali ya Tanzania na OPEC Fund For International Development (OFID) wakishirikiana na BADEA. OPEC wametoa milioni 8 na BADEA wametoa milioni 8. Ili kufanikisha mradi huu Serikali ya Tanzania itatoa dola za kimarekali milioni 2.42, Hivyo kufanya mradi huu kufikia jumla ya dola za Kimarekani milioni 18.42.

No comments:

Post a Comment