Tuesday, April 30, 2013

MZANZIBARI ABUNI MITAMBO YA KUZALISHA UMEME MCHEKI HAPA



 Kijana Ali Mohammed, mkaazi wa Tomondo Zanzibar ambaye amebuni na kuendelea na ubunifu wake kwa kutengeneze Mtambo wa kufulia Umeme kwa njia ya Upepo, akitowa maelezo ya mtambo huo kwa waandishi wa habari alipofika katika ofisi za Zanzibar Leo kuonesha mfano wa mashine hiyo inayotumia upepo jinsi ya kufanya kazi ya kutowa umeme wenye uwezo wa kutowa umeme wa KV 40,
 
Amesema hii ni hatua ya pili ya ubunifu wake kwa kutengeza mtambo huo, na kuendelea na ubunifu wake katika  hatua ya tatu kwa kuunda  vifaa vya kuweza kufulia umeme na kuomba ushirikiano wa kupatiwa msaada na Taasisi husika ili kuweza kufanikisha ubunifu wake alioubuni na kuomba msaada kwa Viongozi husika bila ya kupata msaada hadi sasa,
 
Amesema anaendelea na jitihada zake na kuona anafanikiwa katika ubunifu wake na kuomba misaada kwa wahisani, ili kupata mafanikio yake, Vifaa vya kuweza kufanikisha mtambo huu vipi hapa hapa Zanzibar na mafundi wa kuweza kufanikisha upo kinachomtanza ni Fedha za kupata zana za kutengenezea mtambo huo. 
Hii ni Mfano wa Mtambo huo wa kuzalisha Umeme wa Upepo, amesema mtambo huo utakuwa kama hivi na kuweza kutowa huduma ya Umeme. 
 
Mtaalamu huyu anapatikana kwa nambo ya simu hii kwa jina la Ali Mohammed 

0774775189
0773529501

No comments:

Post a Comment