Wednesday, March 20, 2013

WAKRISTO WATAKA SERIKALI IGAWANYE MABUCHA NA MACHINJIO ILI KILA MTU AWE NA UHURU WA KWENDA KUNUNUA NYAMA MAHALI ANAPOTAKAJukwaa la Wakristo  Tanzania (TCF) limemesema  Wakristo wasilazimishwe, kula nyama zilizochinjwa kwa MisingiyaIbada ya Kiislamu kwakuwa Wananchi wa Tanzania ni wa Dini tofauti tofauti na za makabila mbalimbali  na hivyo wameitaka Serikali kutamka wazi kuwa kila Raia ana uhuru wakufuata imani yake katika Swala la Uchinjaji.
Hayo yamesemwa jana na Viongozi wa Jukwaa la Wakristo Tanzania TCF, wakiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Askofu  Peter Kitula, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Askofu Tercisius Ngalalekumtwa , pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentecoste Tanzania  (PCT)   Askofu David Batenzia mbapo walisoma Tamko hilo kwa kupokezana.
Uongozi huo umesema kuwa, Kwakuwa kuchinja wanyama na Ndege ni Ibada kwa Waislamu, Kanisa linapaswa kutambua na kuheshimu jambo hilo na Kuongeza kuwa linaaminika kwamba Sheria ya Nchi inaweka Bayana juu ya Usalama wa nyama hizo kiafya lakini Serikali haielekezi kuwa ni Dini ipi inayopaswa kuchinja mifugo hiyo.

Wakristo hao wameitaka Serikali  iweke wazi utaratibu wa Kugawana Machinjio na Mabucha kati ya Wakristo na Waislamu ili kila Mtanzania  awe huru kujinunulia kitoweo mahali anapotaka sambamba na kuitaka serikali kutimiza hayo Wakristo hawatakuwa wamevunja Sheria yoyote ya Nchi wakiamua kujichinjia kitoweo chao wenyewe.

“Kwa upande Mwingine kwa kuwa tayari zipo bidhaa za Nchi hii ambazo zina Nembo ya Halal na nyingine hazina Nembo hiyo huu ni uthibitisho kuwa, vyakula hivyo vimegawanywa kwa kufuata Misingi ya Imani ya Kidini kwahiyo Kugawana Mabucha na Machinjio sio jambo jipya kwasasa hapa Nchini”, amesema Askofu  Peter  Kitula.
Viongozi hao pia Wameitaka Serikali iimarishe Ulinzi na Mali za wakristo wote Nchini Hasa waliopo Zanzibar maana hiyo ni haki yao kikatiba.

No comments:

Post a Comment