Thursday, March 21, 2013

RAGE AOMBA RADHI WANACHAMA WA SIMBA


Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam Ismail Aden Rage amewaomba radhi wanachama wa klabu hiyo kwa kuwaambia kuwa kikao walichokaa Jumapili katika katika ukumbi wa statlight ni cha harusi .

Akiongea kwa njia ya simu katika kituo kimoja cha radio Rage amesema kuwa anaomba Radhi  kama kuna alimuudhi kwa kutumia lugha ambayo imeoneka sio nzuri Aden alikiita kikao hicho cha wanachama hao kuwa kikao cha harusi jambo lililo zua mijadara na kutokuelewana na baadhi ya wanachama na wengi wao kuudhiwa na kauli kiasi kufikia kumjibu kuwa yeye atakaa cha kitchen Party .


Mwenyekiti huyo ambaye anarejea kesho kutoka Nchini India alipokwenda kufanyiwa matibabu ya uti wa mgongo amesema pindi atakapofika atazungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakbari wa klabu hiyo yenye makao yake makuu  msimbazi jijini Dar es salaam.

Kwa upande mwingine Aden ameipongeza klabu ya Azam kwa kufanya ufunguzi wa kujenga kiwanja kipya cha kisasa cha mpira wa miguu kilicho funguliwa leo na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

Ameongeza kuwa litakuwa somo kwa klabu ya Simba na Yanga kwani japokuwa na ukongwe wa vilabu hivyo hata majengo yao yapo katika hali mbaya .

No comments:

Post a Comment