Friday, March 8, 2013

Prof. Mbarawa ashuhudia Vodacom. Airtel, Tigo, TTCL wasaini kushiriki Mfuko wa Mawasiliano ya Umma

Picture
Mwakilishi wa Vodacom Tanzania Bw.Nguvu Kamando, (Kulia), akiweka saini makubaliano ya pamoja ya kampuni nne za simu za mkononi, kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma jijini Dar es Salaam . Katika mkataba huo makampuni ya Tigo, TTCL, Airtel ambapo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,(Watatu kulia waliosimama), alishuhudia. (Pichan na Mpiga Picha wetu)
Picture
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na makampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania.Airtel,Tigo,TTCL kuweka saini makubaliano ya pamoja ya kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma.
Picture
Baadhi ya wawakilishi wa kampuni za simu za mkononi wakimpigia makofi ,Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,mara baada ya kumaliza kutoa spichi yake wakati wa kuweka saini makampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania,Airtel,Tigo,TTCL kuhusiana na makubaliano ya pamoja ya kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma.
Picture
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Kamugisha Kazaura (Kushoto)Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, Nguvu Kamando, akizungumza baada ya hafla ya kusaini mkataba wa ushiriki wa mfuko wa mawasiliano ya umma, jijini Dar es Salaam, ambapo makampuni manne ya simu za mkononi yameshiriki. Makampuni hayo ni Vodacom Tanzania, Tigo, TTCL na Airtel .

No comments:

Post a Comment