Wednesday, March 27, 2013

MAMA AMFANYIA UKATILI MTOTO WA DADA YAKE NA KUMNYWESHA MKOJO

Picture
Ukatili hauwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja kupambana nao.

Huyu ni binti ZAWAD KARIM (16), mkazi wa Mshindo,  nyuma ya benki ya NBC katika manispaa ya Iringa ambaye amepigwa na kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever Ubamba.  Majirani wamesema kuwa vitu vilivyotumika kumwadhibu vilikuwa ni pamoja na nyaya za simu, mkanda na vipande vya chupa vilivyotumiwa kumchoma.

Inasimuliwa kuwa kisa cha yote hayo ni madai ya Zawadi kuomba aneshwe Baba yake mzazi ili walau aweze kupata pumziko la adha anazozipata kutoka kwa ndugu zake.

Aidha, taarifa za ndani zinasema kuwa Mama yake Zawadi alitupwa akiwa mtoto mchanga na kuokotwa na wasamaria wema na kulelewa na Bibi yake ambaye kwa sasa amefariki dunia.

Watuhumiwa wa tukio hili, Mama mzazi pamoja na Mama mdogo, wanashikiliwa na jeshi la Polisi katika kitengo cha Dawati la Jinsia, kwa mahojiano zaidi.

---
Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Francis Godwin, IRINGA

No comments:

Post a Comment