Tuesday, March 26, 2013

COSTECH NA TAREA KATIKA WARSHA YA KUJADILI JUU YA NISHATI JADIDIFU

Mkurugenzi  Mkazi Kutoka Ubalozi wa Sweden Bi Maria Vanbecrose akiongea na waandishi wa habari katika Warsha kuhusu hali ya Nishati Jaddifu Nchini Tanzania iliyofanyika Leo katika Makao makuu ya Tume ya Sayansi na Teknolojia yaliyopo jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa anaishaurt Serikali kuaminisha Watanzania Juu ya Umuhimu wa Nishati Jadidifu ili  waweze kutumia nishati hiyo badala ya Kutumia Nishati nyingine.
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kwa Kushirikiana na Taasisi ya Wadau wa Nishati Jadidifu Nchini Tanzania (TAREA) Wameandaa Warsha ambapo wadau mbalimbali wa Nishati watabadilishana Mawazo juu ya hali halisi ya Tecknolojia   Jadidifu nchini Tanzania.

Katika Warsha hiyo, wadau watatoa maoni juu ya Mfumo na Mbinu za kukusanya na kuendeleza taarifa kuhusu maendeleo ya Nishati Jadidifu.

Aidha katika Warsha hiyo COSTECH na TAREA watabadilishana makubaliano ya Ushirikiano kati yao juu ya Mambo yote yanayohusu utafiti wa teknolojia ya Nishati Jadidifu.

No comments:

Post a Comment