WANANCHI wa Kijiji cha Zuzu Kata hiyo mkoani Dodoma, Wameiangusha
Serikali ya Kijiji hicho iliyokuwa ikiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti
Peter Mtawale (49) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye ameamua kuiacha
Ofisi yake kwa kosa la kuuza Mlima wa Widete.
Mtawale aliyezaliwa
1963 alikubali kujiuzulu kwa kuutangazia Mkutano wa Hadhara karibuni
mwaka huu baada ya kubanwa na tuhuma nyingi ikiwemo ya kuuza Mlima huo
kwa Mwekezaji ambaye alikiri Serikali yake ilimruhusu uchimbaji wa Rupia
bila kuwaarifu wananchi.
Mbali ya Tuhuma za kuuza Mlima bila
kuwataarifu wananchi na Uongozi wa Kata, nyingine ni pamoja na mauzo ya
Changarawe (Kifusi), Maji, Mchanga, Ufujaji wa Fedha ya Malambo
Mbgani, Ushuru wa Magari, kuingia kwa wageni bila taarifa, Kutoitishwa
kwa Vikao na kusoma Mapato na Mtumizi, Milio ya Milipuko, na Viongozi
kufunga Maji bila Mita.
“Kuna Uchochezi ninaofanyiwa na Diwani wa
Kata Awadhi Abdalah (CCM), Mwenyekiti wa Changu (CCM) Omari Kagusi na
Katibu Mwenezi Solo (CCM) ambapo 14.1.2012 walifanya kikao cha Siri
kunijadili bila kunitaarifu,”alisema Mtawale alipohojiwa na kuonekana
anafanya kazi zake kwa kuongozwa na Kigogo mmoja wa Kata anayempotosha.
Alipoulizwa
kwa nini Serikali yake haikuwaarifu wananchi juu ya kuuzwa kwa Mlima
huo hadi wakapatana Mwekezaji akipata anachochimba Mwekezaji atachukua
asilimia 60% na Kijiji asilimia 40% alisema, kwa kuwa vikao vinakaa mara
tatu kwa mwaka ilikuwa wawaarifu Machi, 2013.
Pamoja na kukiri
kuingia mkataba huo mwezi Desemba 2012 alikubali walifanya makosa ya
kutowaarifu wananchi na Uonozi wa Kata, lakini akasema Katibu Tarafa
Joyce Malare ametumwa kutatua mgogoro huo lakini walishindwa kukaa hadi
21.1.2013 kutokana na koramu (akidi) kutokutimia.
Diwani Abdalah
alipoulizwa alikiri kuwepo kwa Mgogoro huo na kusema yeye ametoa Taarifa
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ambaye amesema analifanyia Kazi,
lakini alishangaa Katibu Tarafa kuanza kumuingilia akifanya Kazi za
Kisiasa ili kumgonganisha na Wananchi Jambo alilosema hawezi kuvumilia
na kukubali wananchi wadhulumiwe haki yao.
Aidha Katibu Tarafa
Malare alipoulizwa na mwandishi amefikia wapi katika utatuzi wa mgogoro
huo, hakuonesha ushirikiano na kuanza kumponda Mwandishi, “…nani
kakwambia umbeya huo? ...Kwa utaratibu nikifanya kazi nampelekea mkubwa
wagu siyo wewe!!”
Alimwagika maneno yasiyo na staha bila kujua
Mwandishi alimhoji Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Lephy Benjamini juu ya
mgogoro na kujibiwa anaushughulikia Malare.
No comments:
Post a Comment