Wednesday, February 13, 2013

WIZARA YA ELIMU YATANGAZA AJIRA KWA WALIMU WAPYA

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi leo imetangaza Ajira ya walimu wapya wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu Tanzania Bara mwaka 2012/2013.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Katika wizara hiyo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa amesema kuwa jumla ya Walimu 26,537 wameajiriwa serikalini, kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Amesema kuwa walimu wa Ngazi ya Cheti walio ajiriwa kuwa ni 13, 568 kati ya walimu 13,527 wamepangwa kufanya kazi katika shule za msingi zilizopo kwenye halmashauri na walimu 41 wamepangwa katika shule za msingi za Mazoezi zilizo chini ya Wizara.

Ameongeza kuwa jumla ya walimu wa Sekondari na vyuo vya ualimu walio ajiriwa ni 12,973 wakiwemo walimu wa Shahada 8887 na wa Stashahada 4,068.

Walimu, waliopangwa kufundisha shule za Sekondari zilizo chini ya Halmashauri ni 12, 893 wakati wakufunzi wa vyuo vya ualimu ni 59 na walimu 21 wamepangwa kufundisha shul;e za mazoezi zilizop chini ya wizara ya Elimu.

Aidha Dkt Kawamba amesema kuwa idadi ya Walimu walioajiriwa kwa mwaka 2012/2013 imeongezeka kwa asilimia 11 sawa na walimu 2630 ikilinganishwa na walimu23,907 walio ajiriwa mwaka uliopita.

No comments:

Post a Comment