DAR ES SALAAM, Tanzania
WATANZANIA jana wameungana na
Jamhuri ya Kiislam ya Iran katika
kusherehekea miaka 34 ya mafanikio tangu
mapinduzi yaliongozwa na Kiongozi wa Kidini, Ayatollah Khomen yakumuondoa
madarakani Mfalme Shah Pahlavi mwaka 1979.
Kauli hiyo imetolewa jijini
Dar es Salaam leo na Balozi wa Iran nchini Mehdi Agha Jafari, katika sherehe
hizo ambazo zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje, akiwemo Rais wa
awamu ya pili, Ali Hassani Mwinyi.
Alisema Wairan wanajivunia
mapinduzi hayo kwani yamekuwa chachu ya misingi ya haki katika jamii ambapo pia
yameweza kuifanya nchi hiyo kupiga hatua kimaendeleo hadi kutambulika kimataifa.
Jafari alisema mafanikio
yaliopatikana baada ya mapinduzi hayo ni katika sekta za viwanda, afya,
Teknolojia na upande wa kilimo.
Aliongeza kuwa nchi hiyo hivi
sasa imefanikiwa kuzalisha awataalam wake, ambao wamefanikiwa kurusha vyombo
vya kisayansi kwenda anga za juu.
“Hivi sasa nchi yetu
inaviwanda vya kutengeneza dawa mbalimbali ikiwemo za binadamu pia upande wa
kilimo hatuko nyuma tunazalisha zana za kilimo haya ndio mafanikio ya
mapinduzi”alisema Jafari.
Aidha, nchi hiyo iliingia
katika mapambano dhidi ya utawala wa Mfalme Shahah kwa zaidi ya miaka 20
kutokana na dhuluma, kujilimbikizia mali katika familia yake, kuua tamaduni za
Wairan huku akiruhusu tamaduni za nchi za magharibi ambazo ni kinyume na
nchi hiyo.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha, akizungumza kwa niaba
ya Waziri Berdard Membe ambaye yuko Dodoma kwa majukumu muhimu, alisema Tanzania itaendeleza ushirikiano na nchi hiyo, kwani
ushirikiano wa nchi hizo mbili una historia ndefu hususan kwa upande wa Zanzibar.
Vilevile wanaishurukuru nchi
hiyo kwa misaada kwenye maeneo mbalimbli nchini yakiwemo ya Afya, kilimo,
kielimu na mengine.
No comments:
Post a Comment