Wafungwa
wanaotumikia vifungo mbalimbali Mkoani Mbeya wanatembea nusu uchi
kutokana na sare zao kuchakaa na kuondoa hali ya utu wa kibinadamu hali
inayoonesha Wizara ya Mambo ya ndani haiwajali, licha ya Serikali
kuonekana kuboresha maslahi kwa watumishi wake na kuhakikisha wanavaa
sare nzuri.
Uchunguzi
umebaini kuwa wafungwa katika magereza ya Ruanda, Songwe na Kawetere
ndio yaliyo katika hali mbaya na kuwafanya baadhi ya ndugu kushindwa
kuwatembelea ndugu zao baada ya wafungwa hao kushindwa kujisetiri kwa
adha hiyo.
Aidha
mbaya zaidi ni pale wanapoamriwa kuchuchumaa chini hivyo wafungwa hao
kuwa na mawazo ya namna ipi waweze kujisetiri maungo yao hasa kwa
wafungwa wa jinsi ya kiume.
Katika
hali ya hewa mkoani hapa ni baridi kali na wafungwa wengi hawana
masweta na hivyo kubaki na sare chakavu ambazo zinahatarisha afya zao na
kuwa hatarini magonjwa ya kifua na vichomi ambavyo vinaweza kusababisha
vifo.
Wakuu wa magereza katika magereza hayo hawakuweza kuzungumzia lolote wakidai kuwa wao sio wasemaje wa Jeshi la magereza.
Hata
hivyo juhudi za kumpata msemaji wa Jeshi la magereza makao makuu
ziligonga ukuta baada ya kuambiwa kuwa msemaji yupo safarini na
haijulikani siku ya kurudi kazini.
No comments:
Post a Comment