Monday, February 11, 2013

TANZANIA YAPETA MAAJABU SABA YA AFRIKA

Mahmoud Ahmad,Arusha
TANZANIA imepata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika kupitia vivutio vyake bora vya utalii  vya  Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti ambayo ndio iliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi nyingine yeyote.
Akitangaza matokeo hayo jana mjini hapa  rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa nchini Marekani mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda alisema kutokana na Tanzania kuwa na vivutio vya kipekee ndio sababu iliyopelekea kupata ushindi huo.
Akielezea hifadhi ya taifa ya Serengeti alisema kuwa ndio hifadhi ya kipekee iliyopata kura nyingi na kutokana na tabia za misafara ya wanyama wanaohama kwa msimu.
Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo alisema kuwa nchi za Afrika zinavivutio vingi vya utalii na fursa kubwa ya kukuza pato kupitia utalii huo.
Alisema anaamini kutokana na sifa ambayo Tanzania imezipata kupitia vivuti vyake vitatu itaendelea kuvitunza kuhakikisha kuwa  vinavutia zaidi watalii na kuongeza pato la taifa.
“Afrika ina vivutio vingi  vyenye kuvutia hivyo kila nchi ni lazima ijivunie rasilimali hizo kwa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
“Alisema kwa Tanzania ni bahati ya pekee kwa kuweza kupata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika  ambazo ni za Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro pamoja na hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo ni wajibu wa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema Pinda.
Alisema kuwa iwapo watanzania wataendeleza tabia ya utunzaji wa vivutio vilivyopo nchini, nchi itaendelea kupata sifa duniani kote.
Naye Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Dk, Alan Kijazi alisema mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya kushinda na watanzania waendelee kuutunza.
Akizungumzia kuhusiana alisema kuwa hifadhi hiyo imeshinda kwa kuwa kuwa na wanyama wa kila aina kama Big Seven, Simba, tembo, Viboko, Nyati, Vifaru, Sokwe na Mamba.
Mbali na Tanzania Dk.Imler alivitaja vivutio vingine vilivyoshinda kuwa ni Red sea Reefs, Okavango Inland  delta iliyopo nchini Botwasana, Sahara Desert na River Nile.
Aidha Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ushindi huo ni historia kubwa duniani na kwamba ni jambo la watanzania wote kujivunia.
Pia aliwashukuru wananchi walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na kuviwezesha kuingia katika ushindi kwa mara tatu.

No comments:

Post a Comment