ROSE MIGIRO NDIYE MKUU WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania.
Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini
leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka
huu wa 2013.
Mheshimiwa Asha
Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment