Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine mbalimbali kesho
wanatarajiwa kuwaongoza maelfu ya waombolezaji katika
mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Askofu Dk Thomas Olmorjor Laizer (69).
Askofu Laizer aliyefariki dunia katika hospitali ya Seliani Mjini Arusha Februari 7, mwaka huu anatarajiwa kuzikwa katika viwanjavya Kanisa Kuu la KKKT Arusha Mjini.
Rais Kikwete na viongozi wengine wa Kitaifa akiwemo Rais Mwinyi, Rais Mkapa na waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu Sumaye na Lowassa ambao Viongozi tayari wameshawasili mkoani Arusha kwa ajili ya shughuli hiyo.
Mazishi hayo pia yanatarajiwa kuhudhuriwa na na Maskofu wa Kanisa la KKKT kutoka Dayosisi zaidi ya 20, Askofu kutoka Jumuiya ya CCT pamoja na Maskofu kutoka Kanisa Katoliki.
Viongozi wa madhehebu ya KKKT kutoka nchini Marekani na Ujerumani pamoja na Vyuo mbalimbali alivyowaji kusoma Marehemu Askofu Dakta Thomas Ole Laizer nao tayari wamewasili Mkoani Arusha kuhudhuria
mazishi ya Kiongozi huyo.
Ibada ya mazishi itakongozwa na Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Dk Alex Malasusa.

No comments:
Post a Comment