Monday, February 18, 2013

NIMRI WASEMA UKOSEFU WA MAABARA ZA KUTOSHA PAMOJA NA VIFAA VYAKE NI CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO

Mkurugenzi wa kuratibu na kukuza utafiti Dkt Julius J. Masaga

Tatizo la miundombinu ya maabara, vifaa vya maabara  na majengo ya kutosha limetajwa kamachangamoto kubwa inayoikumba secta ya utafiti Tanzania jambo linalosababisha kutokufanya vizuri sana kwa sector hiyo

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam, na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya taifa ta utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini (NIMRI) Dkt, JULIUS MASAGA wakati akifungua semina ya siku tatu inayowahusisha wadau wa maswala ya tafiti na watafiti yenye lengo la kukuza uelewa na kujikumbusha mambo mbalimbali yanayohusiana na tafiti

Dkt, MASSAGA amesema pamoja na sector hiyo kuonekana inafanya vizuri ikiwa ni pamoja na watafiti wengi kuongezeka lakini changamoto bado zipo huku akitolea mfano kama ukosefu wa rasilimali fedha, na nyingine kubwa kuwa ni ukosefu wa miundombinu ya majengo na maabara za kutosha huku akisema maabara zilizopo nchini pia hazina vifaa vya kutosha

Katika semina hiyo MASSAGA amesema lengo kuu la Semina hiyo, ni kuwapa watumishi hao uelewa na mafunzo ya kazi za maadili na pia kupitia tafiti na pia kuzipa tafiti vibali.

No comments:

Post a Comment