Machafuko
makubwa yametokea leo katika kijiji cha Buseresere Wilayani Chato
Mkoani Geita kati ya waslam na wakristu na kupelekea watu 10 kujeruhiwa
vibaya kwa mapanga huku mchungaji wa kanisa la Pentekoste Assemblies of
God Mathayo Kachila (45) akipoteza maisha kwa kuchinjwa na watu
wanaodaiwa ni waumini wadini ya kiislam kisha mwili wake kutelekezwa
kwenye vibanda vya maduka ambavyo vilikuwa jirani na eneo hilo.
Habari
za kaminika eneo la tukio hilo lililotokea majira ya asubuhi zimeeleza
kuwa chanzo cha machafuko hayo ni watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wadini ya
kiislam kuvamia bucha lililokuwa likiwauzia nyama wakristo wa kijiji
hicho waliokuwa wamepanga foleni kwa wingi kusubili huduma hiyo.
Imeelezwa
kuwa Wakristu hao walikuwa wamechinjia ng'ombe mmoja na mbuzi wawili
eneo la Kanisani kabla ya kuleta nyama hiyo katika bucha hilo lililopo
eneo la Buselesele Sokoni na ndipo walipokumbana na kadhia hiyo ya
waislamu.
Tukio
hilo lilianza majira ya saa 2 asubuhi muda mfupi baada ya nyama
kuwasili katika bucha hilo la wakristu kwa ajili ya kuuzwa jambo
linalodaiwa liliwakera waislam ambao waliivamia bucha hiyo kwa lengo la
kuifunga.
Wakati
wakristo wakitafakari uwepo wa waislam kwenye bucha lao lililpambwa kwa
maandishi BWANA YESU ASIFIWE,YESU NI BWANA, ndipo waislam ambao kwa
wakati huo walikuwa wametapakaa mtaani kwa lengo la kuhamasishana
waliongezeka eneo lilipo bucha hilo na kisha kuimwagia nyama iliyokuwa
kwenye bucha hilo vitu vinavyodaiwa kuwa ni sumu.
Kutokana
na hali hiyo wakiristo walionekana kukerwa na kitendo cha waislam
kuimwagia nyama hiyo vitu hivyo na kisha mapambano yalianza baina ya
wakristu na waislam ambapo mbali na wakristu kutumia mawe waislamu wao
walitumia mapanga na majambia.
Hata
hivyo wakati mapambano hayo yakiendelea mchungaji huyo ambaye kwa sasa
ni marehemu alifika eneo la tukio ili kujua kulikoni na ndipo naye
alipojikuta akishambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za kichwa chake
na alifia njiani wakati akikimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Geita
kwa matibabu zaidi.
Mbali
na mchungaji huyo kupoteza maisha,wengine waliojeruhiwa ni pamoja na
Said Ntahompagaze(45),Sadick Yahaya(40),Yasin Rajab(56),Vicent
Damon(22),wote wakazi wa Buselesele na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina
moja la Ramadhani ambaye yuko mahututi katika wodi namba nane katika
hospital ya wilaya ya Geita.
Hata
hivyo watu wengine watano ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara
moja walitibiwa na kuruhusiwa kutokana na hali zao kuwa nzuri.
Jeshi
la polisi Wilayani Chato na Geita lilifika eneo la tukio hilo majira ya
saa 4:30 na kukuta uharibifu mkubwa umekwishafanyika ikiwa ni pamoja na
kukuta duka la Mwenyekiti wa BAKWATA wilaya ya Chato Yusuph Idd
linalotumika kwa biashara ya M-Pesa na vinywaji baridi likiwa
linateketea kwa moto uliodaiwa kuwashwa na waumini wa dini ya kiislam.
Mkuu
wa Wilaya ya Chato Ludorick Mpogolo aliyefika eneo la tukio muda mfupi
baada ya polisi kuwasili eneo hilo mbali na kusikitishwa na kitendo
hicho aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia njia sahihi za kutatua mgogoro huo ambao unakuwa kwa kasi kila kukicha.
Akizungumza
kwa njia ya simu na gazeti hili mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said
Magalula mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo, alionyesha kukerwa
na watu ambao wanafurahia vurugu zisizo na msingi na kuonya
kuwashughulikia wale wote watakaobainika ni wachochezi wa masuala ya
kidini.
No comments:
Post a Comment