Akina mama wajasiriamali wa kata ya Kwa Mndolwa Wilayani Korogwe
wakimtumbuiza Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo(hayupo pichani)
muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuwasili katika kijiji cha Kwa
Mndolwa mwishoni mwa wiki kuongoza hafka ya kukabidhi mikopo nafuu kwa
wanawake zaidi ya 90 iliyotolewa na Vodacom Foundation kupitia mradi
wake wa Mwei.
Mpango
mahsusi wa kampuni ya Vodacom wa kuwawawezesha wanawake wajasiriamali
wadogo kiuchumi vijijini umeendelea kutoa tumiani kwa jasiriamali zaidi
wanawake ambao ukuzaji wa mitaji ya biashara wanazoziendesha sio wa
uhakika kutokana na kukosa uwezo wa kukopesheka kutoka taaisi za fedha.
Ikiwa tayari imeshawanufaisha wanawake zaidi ya 7,000 nchini mradi wa Mwei mwishoni mwa wiki umewafikia wanawake zaidi ya 250 katika Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga ambao wamewezeshwa mikopo midogomidogo ya kati ya Shilingi 50,000 na 100,000.
Akiongea katika kijiji cha Kwa Mndolwa ambapo wanawake zaidi ya 90 wamenufaika na mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo aliwataka wanawake hao kuhakikisha uchukuaji wa mikopo hiyo unatimiza malengo na mikakati ya kibiashara na pia uombaji wa mikopo hiyo na hatimae kujiinua kiuchumi.
Gambo amesema katika hali ya kawaida sio jambo rahisi kupata taasisi inayoweza kuwakopesha wajasiriamali wadogo bila ya riba wala masharti yanayoweza kumpa mkopajo ugumu na hivyo njia muhimu ya kuthamini ujasiri wa Vodacom ni kwa wanawake kutumia vema fursa hiyo kujiinua kiuchumi.
Amesema zimekuwepo taasisi nyingi zinazopita ikiwemo vijijini kutoa mikopo kwa wanawake lakini riba na masharti ya mikopo hiyo mara kadhaa imekuwa michungu kwa wakopaji na wakati mwengine kuwa mzigo kwa wakopaji badala ya neema ya kukuza mitaji ya biashara.
"Zipo taasisi nyingi tu zinakuja kwenu kwa nia ya kuwakopesha lakini najua namna ambavyo masharti ya mikopo hiyo inavyokuwa mzigo kwenu, leo Vodacom inawapatia mikopo isiyo na mashatri wala riba ni matumaiani yangu kwamba mtaitumia vizuri kutimiza malengo yenu ya kujikwamua kiuchumi."Alisema Gambo
"Vodacom imeonesha nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania pasi na kuonesha ubaguzi kwani wangeweza kuwakopesha wateja wake tu lakini hawafanyi hivyo uwe mteja ama la wewe kwao ni mtanzania na wapo tayari kukusaidia kitendo hiki kinachangia pia katika kujenga umoja ndani ya jamii zetu."Aliongeza Mkuu huyo wa Wilaya ya Korogwe.
Katika kuwapa changamoto ya kukuza biashara zao Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wajasiriamali hao kuwa wakweli kwa Vodacom juu ya maandeleo ya biashara zao wakati wa kurejesha mikopo hiyo utakapaonza kwani njia hiyo itawasaidia kupata msaada juu ya changamoto zinazowakabili.
"Kampuni ya Vodacom ni kampuni inayojali maisha ya watanzania na ndio maana ipo hapa leo kuwawezesha mikopo ya kukuza mitaji yenu ya biashara hivyo lazima muwe wakweli katika urejeshaji na hata kama ikitokea kuna tatizo basi kuweni wawazi kwao mapema ili mpate msaada badala ya kuficha tatizo,” amesema Gambo
Aidha, Gambo ameitaka jamii kuiunga mkono kampuni ya Vodacom kutokana na namna inavyojali jamii kwa ujumla kwa kusaidia katika miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya na maji na akina mama wajasiriamali.
Kwa upande wake Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon amesema azma ya Mwei ni kuwainua kiuchumi wanawake wajasiriamali hususan wa vijijini ili kuwawezesha kuchangia kipato katika kaya na hivyo kuharakisha kasi ya maendeleo ndani ya familia.
Amesema mradi huo wa Mwei (M-pesa Women Empowerment Initiative) umeonesha mafanikio makubwa katika azima yake pamoja na kupata ushirikiano wa wanawake wanaokopeshwa ambao wamekuwa wakirudisha mikopo hiyo vizuri na hivyo kuwezesha wanawake zaidi kunufaika.
"Wote tunatambua kuwa ukimwezesha mwanamke umeiwezesha familia tutaendelea kuongeza mkazo katika azma yetu ya kuwasaidia wanawake ingawa pia tunatambua mchango wa wanaume na ndio maana tunasisitiza kuwa wanaonufaika na mikopo hii bado wanawajibu wa kuheshimu nafasi yao kama mwanamke katika familia na jamii."Amesema Grace
Amesema Mwei imeshawafikia wanawake zaidi ya 7,000 nchi nzima Bara na Visiwani klwa kuwapatia mikopo ya kupanua mitaji ya baishara zao ndongondogo na kwamba lengo ni kuwafikia wanawake zaidi kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua vipato na kuondoa umasikini kwa Watazania.

No comments:
Post a Comment