NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU WA UJASIRIAMALI.
NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI ( MARCH 2013 INTAKE )
(INTAKE HII NI MAALUMU KWA WAOMBAJI WANAOTAKA KUWA WAALIMU WA UJASIRIAMALI KATIKA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI & VIJIJINI KWENYE WILAYA WANAZO ISHI)
NAFASI ZA MAFUNZO NA KAZI ( MARCH 2013 INTAKE )
(INTAKE HII NI MAALUMU KWA WAOMBAJI WANAOTAKA KUWA WAALIMU WA UJASIRIAMALI KATIKA MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI & VIJIJINI KWENYE WILAYA WANAZO ISHI)
Taasisi ya RafikiElimu Foundation inapenda kuwatangazia vijana wa kitanzania nafasi za mafunzo na kazi kama ifuatavyo :
KOZI ITAKA YO FUNDISHWA: UALIMU WA UJASIRIAMALI.
SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI:
Awe mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45.
Awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne, sita na kuendelea.
Aliye na utashi na malengo ya kufanya kazi kama MWALIMU WA UJASIRIAMALI kwenye Mradi Wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini.
Anayeweza kusoma na kuelewa kwa njia ya masafa marefu.
Awe anaishi katika mojawapo kati ya wilaya zifuatazo ; Arusha Mjini, Arumeru, Moshi Mjini, Ilala, Kinondoni, Temeke, Babati, Kigoma Mjini, Bagamoyo, Kisarawe, Kibaha Mjini, Nyamagana, Ilemela, Nansio-Ukerewe, Shinyanga Mjini, Kahama, Iringa Mjini , Njombe, Mafinga Mjini, Mtwara Mjini, Morogoro Mjini , Dodoma Mjini, Tanga Mjini, Rungwe( Tukuyu ), Mbeya Mjini, Tandahimba, Lindi Mjini, na Mkuranga.
DHUMUNI LA KOZI HII: Dhumuni kuu la mafunzo haya ni kuwaandaa wahitimu kufanya kazi kama WAALIMU WA UJASIRIAMALI katika Mradi Wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini unaoratibiwa na Taasisi.
MUDA WA MAFUNZO: Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa miezi mitatu. Mwezi mmoja utakuwa ni mafunzo kwa njia ya nadharia na miezi miwili itakuwa ni mafunzo kwa njia ya vitendo ambayo yatafanyika mashuleni na kwenye vituo vya mafunzo ya ujasiriamali.
BAADA YA KUHITIMU: Wahitimu wa mafunzo haya, watapata nafasi ya kufundisha somo la Ujasiriamali mashuleni na katika vituo vya ujasiriamali vilivyopo katika wilaya zao. .
ADA YA MAFUNZO: Ada ya mafunzo haya maalumu ni shilingi elfu 35 tu kwa mwezi.
Tuma maombi ya fomu ya kujiunga na mafunzo-kazi haya kupitia barua pepe yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.com
Maombi yaelekezwe kwenda kwa :
Mkurugenzi Mtendaji,
RafikiElimu Foundation,
Centre For Distance Learning Programme.
S.L.P 35967,
Dar Es salaam.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 08 MACHI 2013.
Mafunzo yataanza, tarehe 14 MACHI 2013.
N.B: Tutachukua wanafunzi wachache kutoka katika wilaya tajwa hapo juu, hivyo idadi ya wanao hitajika ikikamilika mapema, tutasitisha kupokea maombi mapya.
Kwa maelezo zaidi, tembelea: rafikielimu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment