DAR ES SALAAM, Tanzania
HATIMAYE aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Mserbia
Milovan Cirkovic, ameamua kutua nchini ili kuhakikisha Uongozi wa klabu hiyo
unamlipa madai yake yaliyosalia mara baada ya kuvunja nae Mkataba.
Milovan amesema,
ameamaamua kuja nchini kudai stahiki zake mara baada ya kuona uongozi
ukishindwa kulitatua suala hilo.
Alisema amekuja na hatoondoka mpaka atakapoakikisha
analipwa fmadai yake ambayo anayadai na kudai kushangazwa na viongozi kushindwa
kupokea simu zake anapowapigia.
Milovan amefikia katika juzi Hoteli ya
Spice jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwaona viongozi wa Simba ili apate
haki yake na kurudi kwao Serbia.
Kocha huyu alitupiwa vilago kwa madai ya timu yake
kutofanya vizuri katika baadhi ya mechi zake mwishoni mwa raundi ya kwanza na
nafasi yake kutwaliwa na Mfaransa Patric Lieweg.
Katika
hatua nyingine mashabiki wa Simba waliohudhuria pambano la kimataifa
kati ya Stars na Cameroon walimbeba juju kocha huyo mara baada ya
kumalizika kwa pambano hilo huku wakiimba 'huyu ndiye kocha wetu huyu
ndiye kocha wetu' babu hatumtambui.
No comments:
Post a Comment