Mkurugenzi wa taasisi huru ya
Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki Jawad Jaffer akimkabidhi
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji
cheti cha tuzo ya ubora na thamani ya nembo kwa kampuni zinazotoa huduma
bora kwa walaji katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Taasisi
huru ya Superbrands ambayo ni kubwa kuliko zote duniani, inayoratibu
ubora na thamani ya nembo kwa kampuni zinazotoa huduma bora kwa walaji,
leo imekabidhi vyeti vinavyotambuliwa kimataifa vya utambuzi wa ubora wa
bidhaa kwa kampuni zilizofanya vizuri nchini Tanzania kwa mwaka
2013/2014.
Tuzo za Superbrands ni miongoni mwa tuzo zenye thamani kubwa na zinazoleta heshima ya pekee ndani ya kampuni.
Hii ni mara ya tatu kwa tuzo hizo kutolewa ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki tangu kuanzishwa kwake yapata miaka mine iliyopita.
Uamuzi na hatimaye utoaji wa tuzo husika unatoka baraza huru la wataalamu waliobobea katika masuala ya biashara, lakini lengo hasa likiwa ni ni kustawisha na kuhamasisha ari katika utoaji huduma zinazo zingatia ubora.
MeTL imekuwa moja wapo kati ya Makampuni yaliyopokea vyeti vya tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya tatu hapa nchini.
---
Habari, Picha via Mo Blog Team

Mkurugenzi kutoka taasisi ya Superbrands ukanda wa Afrika Mashariki,
Jawad Jaffer akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha
ya kampuni zilizotunukiwa hadhi ya Superbrands wakati wa hafla ya
kukabidhi vyeti vya tuzo za ubora na thamani ya nembo kwa makampuni bora
2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Raha Aashiq Sharrif (Kulia) akiwa
Mwakilishi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Raha Preetkamal Bansal ( wa
pili kulia) wakati wa hafla fupi ya Superbrands kukabidhi vyeti kwa
makampuni bora kwa mwaka 2013/14 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhaville ( wa pili kulia)
aliyembatana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha IPP Bi. Joyce Luhanga (
wa tatu kulia) wakati wa hafla ya utoaji wa cheti cha tuzo ya ubora na
thamani ya nembo iliyoendeshwa na Taasisi ya Superbrands.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji
akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment