ALIYEKUWA
Askofu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini
Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer anatarajiwa kuzikwa Ijumaa Februari 15,
2013.
Kwa Mujibu
wa Taarifa maalum iliyotolewa na Kamati ya Mazishi ya KKKT na Familia ya
Marehemu, inasema kuwa Marehemu atazikwa katika eneo la Kanisa Kuu mjini Kati
Arusha.
Aidha
taarifa hiyo ambayo Father Kidevu Blog imeipata inasema kuwa waumini na
Washirika wa Kanisa Kuu na makanisa yote ya KKKT nchini, Wananchi, ndugu jamaa
na marafiki watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa marehemu
kuanzia Alhamisi Alasiri ya Februari 14, 2013.
Taarifa
hiyo iliongeza kuwa Mwili wa Askofu Laizer utalala Kanisani hapo hadi Ijumaa ya
Mazishi.
Marehemu
Askofu Thomas Laizer alizaliwa Machi 10, 1945 katika Kijiji cha Kitumbeni
Arusha na baade kupata elimu yake ya msingi hadi darasa la nane Longido na
kumaliza mwaka 1965.
Askofu
Laizer, aliendelea na masomo yake ya juu ndani na baade kujiunga na masomo ya Theolojia
katika chuo cha Makumira na baade kuongeza masomo nchini Marekani.
Marehemu
wakati wa uhai wake alikuwa Mwinjilisti, Mchungaji katika makinisa mbalimbali
nchini na baade kuwa Mkuu wa Jimbo na Mkuu wa Sinodi na baade kuwa Rais wa
sinodi kabla ya kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa Kwanza wa Dayosisi ya Arusha
ambayo kwa sasa ni Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Marehemu
Baba Askofu Thomas Laizer ameacha mjane watoto wanne na mjukuu mmoja.
Nae Waziri Mkuu Mstaafu
Edward Ngoyai Lowasa amesema kuwa Kanisa na jamii limempoteza kiongozi na
mpigania maendeleo ya jamii kiroho na kimwili.
“Tumepoteza
kiongozi wa kiroho na kijamii,amehusika katika kuelimisha jamii kwa kuanzisha
shule nyingi za Sekondari,amehusika pia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Arusha
Lutheran Medical Center,zahanti na vituo vya afya katika vijiji kadhaa
Mkoani Arusha pamoja na hoteli ya Corridor springs”alisema Lowasa.
Aliwataka waumini wa
kanisa la KKKT kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na
kiongozi wao.
"Natoa pole
nyingi kwa familia ya marehemu Baba Askofu Laizer na kanisa la KKKT kwa
ujumla wake,lakini askofu Laizer atakumbukwa kwa utumishi uliotukuka katika
siku za uhai wake"alisema Lowasa akihojiwa na kituo cha radio cha kitaifa
cha Radio one asubuhi ya leo.
No comments:
Post a Comment