
………………………………………………….
Watanzania wametakiwa kuacha mawazo potofu juu ya mgawanyo wa rasilimali
zilipo nchini kwa sababu zinatumika kwa ajili ya wananchi wote pasipoupendeleo.
zilipo nchini kwa sababu zinatumika kwa ajili ya wananchi wote pasipoupendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Mhongo
wakati akitoa ufafanuzi kufuatia maandamano yaliyofanyika mkoani Mtwara kwa
madai kuwa ya gesi inayochimbwa mkoani humo kutowanufaisha wananchi wa
mikoa ya Lindi na Mtwara.
Profesa Mhongo amesema maandamano kama hayo yanaweza kuligawa taifa kwa
sababu kila mkoa unatoa rasilimali zake ambazo zinatumika na wananchi wa
mikoa yote bila kujali ukanda wa mikoa husika.
Waziri huyo amesema endapo wananchi wa kila mkoa wataandamana ni hatari
kwa amani na utulivu na ustawi wa wananchi.
Waziri Mhongo amewataka wanasiasa wanatakiwa kuangalia maslahi ya kiuchumi
kwa Taifa badala ya kuwapotosha wananchi na kusababisha mivutano isiyokuwa
ya lazima katika jamii.
Serikali imesema kuwa gesi asilia iliyogunduliwa Mtwara imekuwa ikitumika
kuzalisha umeme wa megawati 18 ambapo mikoa ya Lindi na Mtwara hutumia
kiasi cha Megawati 12 pekee.
Profesa Mhongo amesema serikali inaamini ujenzi wa bomba la gesi asilia
kutoka Mnazi Bay mpaka jijini Dar es Salaam utalinufaisha zaidi taifa kwa
kutumiwa katika viwanda,taasisi na matumizi ya kawaida majumbani.
nA fULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment